TAARIFA YA UKOSEFU W...
TAARIFA YA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI
17 Aug, 2024

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MUSOMA (MUWASA)

Taarifa kwa Umma:

YAH: UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI 

MUWASA inawatangazia Wateja wake kuwa kuna ukosefu wa huduma ya Maji leo tarehe 17.08.2024. Hii imesababishwa na matengenezo ya bomba kubwa eneo la Musoma Bus.

Maeneo yatakayoathirika ni Nyasho, Nyakato, Baruti, Machinjioni na Majengo

Huduma itarejea mara baada ya matengenezo kukamilika

MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa Umma leo tarehe 17.08.2024