TAARIFA YA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI
14 Dec, 2024
MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MUSOMA (MUWASA)
Taarifa kwa Umma:
YAH: UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI
MUWASA inawatangazia Wateja wake kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji leo tarehe 14.12.2024 kwa sababu ya kupasuka kwa bomba kubwa linalopeleka maji kwenye tank la Bhalima.
Maeneo yatakayoathirika ni Kwangwa A&B, Kiara, Songambele, baadhi maneno ya Rwamlimi, Nyabisare, Bweri Bukoba, Nyabange na Bweri.
Huduma itarejea mara baada ya matengenezo kukamilika
MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa Umma leo tarehe 14.12.2024