TAARIFA YA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI
MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MUSOMA(MUWASA)
YAH: UKOSEFU WA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) inawataarifu wateja wake kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa siku ya kesho Ijumaa tarehe 10 Januari 2025 kwa sababu ya kupasuka kwa bomba kubwa eneo la Makoko Jeshini.
Maeneo yatakayoathirika ni mitaa yote ya manispaa ya Musoma , kata ya Etaro, Kijiji cha Nyabange na kata ya Mkirira.
MUWASA inawaomba wateja wake kuhifadhi maji na kuyatumia kwa uangalifu.
Huduma itarejea mara baada ya matengenezo kukamilika.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Kwa Mawasiliano zaidi, tafadhali piga simu namba 0800110108 bure.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma - MUWASA
09 Januari, 2025