TAARIFA YA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KANDA YA MUGUMU
30 Jan, 2025
MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MUSOMA (MUWASA)
Taarifa kwa Umma:
YAH: UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
MUWASA KANDA YA MUGUMU inawatangazia Wateja wake kuwa kuna upungufu wa huduma ya Maji kwenye baadhi ya maeneo kwa sababu ya kutokea hitilafu ya mitambo inayosukuma maji.
Maeneo yatakayoathirika ni Mitaa yote ya Mugumu mjini
Huduma itarejea mara baada ya matengenezo kukamilika.
MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa Umma leo tarehe 30.01.2025