TAARIFA YA UKOSEFU W...
TAARIFA YA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI MUGUMU
09 Apr, 2025

MUWASA kanda ya Mugumu inawatangazia Wateja wake kuwa kuna upungufu wa Maji leo Jumatano tarehe 09/04/2025 kutokana na  kupasuka kwa bomba kubwa linalosambaza maji Mugumu.

Hali hii itasababisha upungufu wa maji kwa baadhi ya maeneo na mengine kukosa kabisa huduma ya maji.

Maeneo yatakayoathirika ni Bomani misitu, Chamoto, Sedeco na Hospital ya Wilaya  Kibeyo.

Huduma itarejea baada ya matengenezo kukamilika

MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.