UPUNGUFU WA UPATIKANAJI WA MAJI TARIME MJINI
27 Sep, 2024
Taarifa kwa Umma:
YAH: UPUNGUFU WA UPATIKANAJI WA MAJI TARIME MJINI
MUWASA inawatangazia Wateja wake kuwa kuna upungufu wa Maji kutoka katika chanzo cha Maji ya Chemichemi Nyandurumo hii imesababishwa na hali ya kiangazi iliyopo kwa sasa. Hali hii imepelekea kuwepo kwa upungufu wa upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo katika Mji wa Tarime Mjini.
Maeneo yanakayoathirika ni Bombani, Mjini kati na Buhemba.
Huduma itarejea mara baada ya hali ya kiangazi kupungua
MUWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Tangazo hili limetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma - MUWASA Tarehe 27.09.2024