MD MUWASA ametoa zawadi ya motisha kwa waliofanya vizuri Julai 2025

MKURUGENZI MTENDAJI MUWASA ATOA ZAWADI YA TSH. 1,200,000/= KWA WATUMISHI 12 WALIOFIKA LENGO LA MAKUSANYO LA 90% KWA MWEZI JULAI 2025
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), Mhandisi Nicas Mugisha, amefanya kikao kazi cha Watumishi wote katika eneo la ofisi leo tarehe 12/08/2025 ikiwa ni sehemu ya kukumbusha utekelezaji wa majukumu ya kila siku katika utoaji wa huduma ya maji kwa wakaazi wa Manispaa ya Musoma na Kanda zinazosimamiwa na MUWASA.
Aidha, katika kikao hicho Mhandisi Nicas Mugisha amekabidhi zawadi kwa Watumishi waliofanya vizuri zaidi kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa Mwezi Julai 2025.
Watumishi waliokabidhiwa zawadi ni Steven Muhangwa, Zakaria Lawi George, Abdalla Bwire Maregesi, Cecilia Lucas, Mariam Charles, Seme Evarist, Yuster Kapinda, Milembe Katemi, Happiness Richard Dominick, Thomas Phares Kumila, Geofrey Rujomba na Dominick Gitanuke.
Watumishi hao waliofanya vizuri zaidi wamepata zawadi pamoja na pongezi ili kutoa Motisha na hamasa kwa Watumishi wote kufanya kazi kwa bidii zaidi.
Mhandisi Nicas Mugisha ametoa kiasi cha shilingi milioni Moja na laki Mbili kwa Watumishi 12 waliofikia lengo la makusanyo kwa mwezi Julai 2025.
MUWASA kazi inaendelea