MUWASA yatoa vyeti v...
MUWASA yatoa vyeti vya pongezi kwa baadhi ya wateja wanaolipia bili zao kwa wakati.
09 Oct, 2025
MUWASA yatoa vyeti vya pongezi kwa baadhi ya wateja wanaolipia bili zao kwa wakati.

MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA: MUWASA YATOA VYETI VYA PONGEZI KWA WATEJA WANAOLIPA BILI ZAO KWA WAKATI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) Imetoa vyeti vya pongezi kwa baadhi ya Wateja wanaolipa bili za maji kwa wakati.

Hayo yamesemwa leo tarehe 08 Agosti, 2025 kwenye Hafla fupi ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyofanyika katika eneo la ofisi za MUWASA.
Baadhi ya Wateja waliohushuria ni mteja Lucia Kitumbo ambaye ameishukuru MUWASA kwa kutoa huduma bora kwa wakaazi wa Manispaa ya Musoma kwa kuwa huduma ya maji inapatikana muda wote kwenye baadhi ya maeneo 
Lucia aliendelea kutoa pongezi kwa MUWASA kwa kuongeza mtandao wa maji kwenye maeneo ambayo huduma haikuwepo "kwa sasa maeneo mengi yana huduma ya majisafi tofauti na kipindi cha nyuma, hongereni sana,

Pia Mteja Emmanuel Werema ameiomba MUWASA ijitahidi kumaliza changamoto zinaowakabili wakaazi wa eneo la Nyabange na Buhare ili eneo hilo liweze kupata maji muda wote.

Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA Mhandisi Nicas Mugisha amewashukuru Wateja waliofika kwenye hafla hiyo kwa kuacha shughuli zao na kujumuika na wana MUWASA.

Aidha Mhandisi Nicas amewaomba Wateja waalikwa kuwa mabalozi wazuri wa MUWASA kwa kutoa taarifa za mivujo ya maji, wizi wa maji na taarifa nyingine zinazohusu huduma ya maji kwa ujumla.

MUWASA imealika baadhi ya  Wateja wanaolipa vizuri bili zao za maji kwa sababu ya kutambua na kuwashukuru kwa kuwa Wateja wanaotimiza wajibu wao vema kwa kulipa bili zao kwa wakati ambapo ulipaji huo huchangia Mamlaka kuendelea kutoa huduma bora na endelevu.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yameanza tarehe 06 Oktoba, 2025 hadi tarehe 10 Oktoba 2025 ikiwa na kauli mbiu isemayo "Dhamira Inayowezekana"

MUWASA inaendelea kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja kwa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali yaliyoandaliwa ikiwa ni pamoja eneo la Bweri center na eneo la Nyakato sokoni, lengo ni MUWASA kuwafikia wateja kwa urahisi.
 
Pia katika Hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA ametoa shilingi milioni 1.1 ikiwa ni  zawadi kwa Watumishi 11 waliofanya vizuri zaidi kwenye makusanyo ya mwezi Septemba 2025.
"JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI NA UTULIVU"